RAPA wa kike kutoka Bongo, Rosary Robert ‘Rosa Ree’, anaendelea kuivuruga Afrika Kusini ‘Sauz’ kutokana na ‘media tour’ anayoifanya kwa sasa kiasi cha kuwa gumzo kwenye media tofautitofauti.

Katika ziara hiyo, Rosa Ree, mbali na kuzungumza Kizungu lakini kwa kiasi kikubwa amekuwa akizungumza Kiswahili, ili kuonyesha kwamba ni Mtanzania, lakini pia amefunguka kwamba kwa sasa kazi zake kwa kiasi kikubwa atakuwa anafanyia nchini humo kwa sababu menejimenti yake inatoka huko.

“Kiukweli Sauz kwa sasa kumekuwa kama nyumbani, ninafanya ziara nyingi kila kukicha na menejimenti yangu imenitengenezea mazingira mazuri ya kufanya kazi. “Baada ya kumaliza tour kuna kitu kikubwa pia kinakuja, mashabiki wangu wakae mkao wa kul a,” alifunguka Rosa Ree, dairekti kutoka Sauz.