DSC_3429
Waziri wa Fedha na Mipqngo Dk.Philip Mpango akipata akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano kwa Umma wakati Waziri huyo alipotembelea Banda la PPRA katika maonesho ya Sabasaba
DSC_3433
Waziri  Fedha na Mipago Dk.Philip Mpango akizungumza katika banda la PPRA wakati alipotembelea Banda la PPRA katika maonesho ya 42 ya Biashara Kimataifa katika viwanja vya Mwalim Julius Nyerere kijiji Dar es Salaam
Waziri Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango ameitaka Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) kuingiza taaasisi za Umma zinazofanya manunuzi makubwa katika mfumo kieletroniki (TANePS) .
Dk.Mpango ameyasema hayo wakati alipotembelea banda la PPRA katika maonesho ya 42 ya Biashara Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.ameesema kwenye manunuzi serikali ndio inapigwa.
Amesema kuwa serikali imekuwa ikipata matumizi makubwa ya manunuzi kutokana na mfumo uliopo.
Amesema PPRA kuanzisha mfumo huo waziingize taasisi za umma zinazofanya manunuzi makubwa.
“Najisikia uchungu fedha zinapotea katika manunuzi sasa ni wakati wa kuingiza taasisi za serikali zinafanya manunuzi makubwa”.amesemMpango.
Nae Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano kwa Umma Bertha Soka amesema katika mfumo huo wamesajili wazabuni 400 huku 10 wakiwasajili katika maonesho ya sabasaba.
Soka amesema kuwa mfumo huo ni suluhu kwa katika manunuzi ya umma na hakuna mtu wa kuweza kukwepa.