Msanii wa muziki anayefanya kazi zake  Mombasa Kenya, Kelechi amefunguka na kudai msanii mwenzake Brown Mauzo hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu.

Siku chache zilizopita Brown Mauzo aliibuka na kufunguka juu ya mapenzi yake kwa msanii wa filamu Tanzania Wema Sepetu na kudai anataka kumuoa jumla jumla.

Kwenye mahojiano na Enews  Kelechi amefunguka na kudai Brown hawezi kumuoa Wema Sepetu wala hata kumuhudumia hawezi:

Huyu Brown ni mtoto mdogo sana hawezi kumpata Wema Sepetu alafu isitoshe ni Dogo sana kwa Wema na pia hana hata hadhi ya kuwa  naye kimapenzi”.

Lakini pia Kelechi amedai Brown amekimbia Mombasa na kurudi Tanzania baada ya kutembea na mke wa Meneja wake.