MSANII maarufu wa vichekesho Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema amekoma kuwa kiongozi misibani kwa sababu ya matusi anayovuna akishika nafasi hiyo. Steve aliiambia Za Motomoto News wikiendi iliyopita kuwa, amekuwa akijitoa kwenye misiba ya wasanii wenzake lakini licha ya wema wake huo amekuwa akivuna skendo za ajabuajabu (kama ulaji fedha za rambirambi) na matusi jambo ambalo linamhuzunisha na kuiathiri familia yake. “Unajua mimi nina watoto, sasa wanapoona yanayoandikwa mitandaoni ya kunitukana na kunifedhehesha kwa vitu vya uongo watanichukuliaje, niseme tu huu msiba wa mtoto Patrick Peter ambaye ni mtoto wa msanii mwenzangu Muna ndiyo wa mwisho, sitajihusisha tena na uongozi; kwenye misiba nitashiriki kama mtu wa kawaida,” alisema Steve