STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa siku zote kwenye maisha yake hapendi kuishi maisha ya mitandao na ndiyo maana hata dera alilolirudia kwenye msiba wa Patrick, hawezi kuacha kulivaa hata siku moja.

Aunt alisema anawashangaa watu wanaomjadili kuwa anarudia nguo na kumtaka anunue nguo kila siku kitu ambacho yeye anaona hakina maana.

“Eti kila sehemu niende na nguo mpya au hata msibani nibadili nguo ina maana nitakuwa sina vitu vingine vya kufanya vya maendeleo zaidi ya kununua nguo kwa ajili ya maonyesho? Watu wasinijadili, sina muda huo wala kufuata wanayotaka wao,” alisema Aunt.