Jay Dee na Gardner Wakutana Uso kwa Uso.... Wasalimiana kwa Kushikana Mikono

Wahenga wanasema milima haikutani lakini binadamu wanakutana! leo kauli hiyo imeonekana baada ya Gadner G. Habash   kupeana mkono na aliyekuwa mkewe Judith Wambura maarufu kama Jdee wakati Jaydee alipokwenda kumpa mkono wa pole Kibonde kufuatia kufiwa na mkewe.

Jaydee aliwasiri nyumbani kwa Kiponde akiongozana na mpenzi wake @Spicymuzik na kuelekea eneo alilokuwa amekaa mfiwa huyo ambaye pembeni yake alikuwepo amekaa Gadner.

Jay D alipofika eneo hilo kwaajili ya kutoa pole kwa wafiwa watu wote akiwemo na Gardner walisimama kwa heshima ili kusalimiana nao naye mwanamama huyo alitoa salamu hiyo kwa wote ikiwemo kwa aliyekuwa mume wake Gardner.

Mke wa Ephrahim Kibonde, Sara Kibonde amefariki dunia usiku wa Jumanne, Julai 10, 2018, katika Hospital ya Hindu Mandal akipatiwa matibabu ambapo leo ibada ya mazishi ilifanyika nyumbani kwa kwake na mwili wa marehemu utaenda kupumzishwa katika makaburi ya Kinondoni.