Familia, ndugu, jamaa na marafiki wa karibu na mtangazaji Ephraim Kibonde wameuaga na kuuzika mwili wa marehemu Sara Kibonde ambaye ni mke wa mtangazaji Kibonde nyumbani kwake, Ubungo Kibangu na kisha baadae kuupumzisha mwili wake katika makaburi ya Kinondoni.

Sara na Kibonde wametimiza miaka 20 ya ndoa uku wakiwa jumla ya miaka 30 ya uhusiano ikiwa wameshawahi kuwa wapenzi miaka 10 kabla ya ndoa na kubahatika kupata watoto watati wawili wa kike na mja wa kiume.

Sara Kibonde amefariki dunia usiku wa Jumanne, Julai 10, 2018, katika Hospital ya Hindu Mandal akipatiwa matibabu.