Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amemteua Naibu Kamishna wa Magereza Phaustine Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imesema kuwa Kamishna Kasike amechukua nafasi ya Dkt. Juma Ali Malewa ambaye amestaafu.

“Rais amemteua Kamishna wa Magereza Phaustine Kasike kuwa Kamishna wa Jenerali wa Magereza na uteuzi huu umeanza leo tarehe 23, Julai 2018″, imesema taarifa.

Kabla ya uteuzi huo Kasike alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA) Ukonga, jijini Dar es salaam.

Kamishna Jenerali wa Magereza Faustine Martin Kasike  mnamo tarehe 25 Mei, 2017 alikuwa miongoni mwa makamishna waandamizi wa Magereza waliopandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John  Magufuli.