Napenda Wanaume Weusi Wanamuonekano Wakiume Kuliko Weupe- Linah

Muimbaji Linah Sanga amezungumza na kusema kuwa anapenda Wanaume Weusi kwani wanamuonekano wakiume zaidi ya wanaume weupe, hata yeye wanaume wake wengi wa zamani walikuwa weusi kwa sababu ndiyo rangi anayovutiwa nayo.

Linah kazugumza hayo baada ya picha inayomuonesha akiwa na mpenzi wake na watu kujadili rangi ya mpenzi wake huyo wakidai kuwa ni mweusi sana lakini Lina yeye kamtetea na kusema yeye ndo kampenda alivyo na isitoshe ma-x wake wote aliotembea nao kama Baraka the Prince, Amini na wengine walikuwa weusi.