Aleksandar Golovin ameipiga chini ofa ya kwenda kujiunga na Chelsea na kuamua kumalizana na AS Monaco 🇲🇨.

Kesho anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na kutambulishwa kwa waandishi habari baada ya kusaini mkataba wa miaka 5. Ikumbukwe kuwa Mkurugenzi wa sasa wa michezo wa Monaco Emenalo aliwahi kuwa mkirugenzi wa michezo wa Chelsea.

CSKA Moscow watapokea kiasi cha €30m kutoka kwa Monaco kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo aliyeng’ara katika michuano ya kombe la dunia 2018 akiwa na timu ya taifa ya Russia.

Ni siku mbili tu zimepita baada ya Fc Barcelona kuipiku As Roma kwa mchezaji Malcom.