Jokate Mwegelo limejiongezea umaarufu mkubwa na wa kutisha katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi ni baada tu ya jina hilo kutajwa katika orodha ya majina 32 ya wakuu wapya wa Wilaya walioteuliwa na Rais Dkt. Magufuli.

Muda mupi tu baada ya uteuzi huo wa Rais Picha, Pongezi na maoni kutoka kwa wafuatiliaji mbalimbali wa mambo vilianza kuonekana kwenye vyanzo tofauti vya habari kila mmoja akizungumza kwa namna yake, ingawa watu wengi walionesha kufurahishwa na hatua ya Rais kutaja jina hilo.

Ni wazi kuwa uteuzi uliofanywa na Raisi Magufuli kumfanya Mwanamitindo, Mwigizaji, na Mjasiriamali Jokate Mwigelo kuwa mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ni wenye hamasa kubwa kwa watanzania wengi hasa wanawake wakitaka kuona safari ya binti huyo mrembo kwenye utendaji kazi na siasa.

Miongoni mwa watu maarufu Tanzania waliompa Pongezi Jokate ni pamoja na Mwanamitindo mwenzake Wema Sepetu ambaye ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuwa, “Hongera sana Mh. DC wa Kisarawe…. @jokatemwegelo , Dada wa Taifa, Green inaendelea jamani” huku Msemaji wa Simba Haji Marana ambaye ameandika “Nakumbuka sana mazungumzo yetuv baada ya ule utenguzi nilijua ni suala la muda tu..hongera DC @jokatemwegelo” pamoja na watu wengine kibao maarufu na wasio maarufu.

Katika Siasa Mnamo Aprili 24 mwaka 2017 umoja wa vijana wa _Chama cha Mapinduzi_ (UVCCM) ulimteua Jokate kuwa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi jumuiya hiyo nafasi ambayo aliitumikia kwa miezi 11 kabla ya kuenguliwa katika nafasi hiyo na Kamati ya Utekelezaji ya Umoja waVijana wa CCM iliyokutana kwa dharura chini ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndg Kheri Denis James mnamo 25/03/2018.

MAISHA na MASOMO.

Jokate Mwegelo alizaliwa mnamo tarehe 20 Machi, 1987, huko mjini Washington, D.C, ambapo wakati huo wazazi wake walikuwa wanafanya kazi. Alikulia jijini Dar es Salaam, Tanzania. Alianza elimu ya msingi katika shule ya Olympio Primary School na baadaye St. Anthony High School, halafu Loyola High School, Dar Es Salaam, Tanzania. Alihitimu katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, ambapo alipata shahada ya sayansi ya siasa na falsafa.

Alikuwa mshindi wa pili katika shinda la Miss Tanzania mwaka 2006. Vilevile alipewa jina la balozi wa Redds fashion na balozi wa gazeti la Citizen, baada ya kupata kura nyingi mwaka huo. Kabla ya Miss Tanzania, alishindana katika Miss Kurasini 2006, shindano ambalo alishinda, kisha kuelekea juu zaidi na kuwa Miss Temeke 2006, ambako pia alishinda.

FILAMU.

Mwaka wa 2007, Jokate alipata kucheza filamu yake ya kwanza iliyojulikana kwa jina la ‘Fake Pastors’, akiwa na Vincent Kigosi, Lisa Jensen, mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2006 na marehemu Adam Kuambiana. Mwaka wa 2008, amecheza katika filamu ya From China With True Love Mwaka wa 2010, alionekana katika filamu ya Chumo, filamu iliyoandaliwa na Media for Development International, kuhusu elimu juu ya ugonjwa wa malaria.

Filamu hiyo ilimwezesha kupata tuzo ya Zanzibar International Film Festival akiwa kama mwigizaji bora wa kike kwa 2011 na kuchaguliwa kama mwigizaji wa Pan-Afrika katika tuzo za 2012 Nigeria Entertainment Awards. Vilevile amepata kuonekana katika mfululizo wa vipindi vya TV na Mwaka wa 2014, amecheza uhusika wa “Ndekwa” katika filamu ya Mikono Salama, ambayo ilimpelekea apate tuzo nyingine ya Zanzibar International Film Festival akiwa mwigizaji bora wa kike kwa filamu za Kiswahili.Mwaka wa 2011, alishinda tuzo ya Zanzibar International Film Festival akiwa kama mwigizaji bora filamu wa kike na Mwaka wa 2017,Jokate Mwegelo aliingizwa katika jarida la Forbes katika Forbes 30 Under 30 kutoka Afrika.

KUHUSU MUZIKI.

Jokate Mwigelo Alishirikishwa katika wimbo wa Japo Nafasi wa Cpwaa akiwa na A.Y. katika wimbo wa Kings and Queen, na Amani, kutoka Kenya. Mwaaka wa 2013, alitoa wimbo wake akiwa na Lucci, uliyoitwa ‘Kaka na Dada, Mwaka wa 2015, akadondosha wimbo wake mwingine akiwa na mwimbaji kutoka nchini Nigeria Ice Prince “ LEO”.

HITIMISHO

Kubwa zaidi ni kwamba pamoja na mambo mengine mnamo jumamosi ya tarehe28/07/2018 Jokate Mwigelo ameanza safari yake ya kuwa mtumishi wa uma ambapo anakwenda kuwaongoza wakazi 95.614 waliopo katika wilaya ya Kisarawe iliyopo mkoani Pwani akiwa kama mkuu wa Wilaya baada ya kuteuliwa na Rais john Magufuli kutumikia nafasi hiyo.