Alichokisema Harmonize kwa Wamachinga Wenzake

Mchumia juani hulia kivulini – Huo ni msemo wa wahenga ambao umekuwa ukionekana kuwa na ukweli ndani yake kutokana na mambo yanavyoonekana katika masiaha.

Miaka mitano sita iliyopita hakuna aliyekuwa anamfahamu Harmonize wala kutegemea kama jina kama hilo litakuja kusikika kwenye Bongo Fleva. Inawezejana kipindi hicho ndio alikuwa anapiga mishe zake jijini Dar es Salaam za kuuza vinjwaji baridi.

Msanii huyo leo hii amekuwa staa mkubwa Bongo na kufahamika sehemu kubwa Afrika. Harmonize ameonekana kwenye video aliyoiweka Instagram akiwa amewatembelea wafanyabiashara ndogo ndogo mjini Kariakoo kwa kuwapa moyo katika kutafuta maisha pamoja na kugawia fedha kama zawadi.

Hit maker huyo wa Kwa Ngwaru hajaishia hapo, katika video hiyo ameandika ujumbe mrefu wa kuwapa moyo watu wasikate tamaa katika maisha. Kupitia mtandao huo, Harmo ameandika:

Miaka (5) iliyopita nilikuwa nafanya biashara za kudunduliza maeneo haya ya #Kariakoo kwa lugha nyengine nilikuwa #Machinga shida, tabu, shuruba, nilizokuwa nikizipitia
M/mungu peke ndie anayefahamu..!! Hata wimbo wangu wa #Matatizo 90% umebeba uhalisia wa maisha yangu sana……!!!! Sina utajiri wowote….!!! ila afadhali niliyoipata najihisi ni mwenye bahati
Sana…!!! Maana maisha ninayoishi
Sikuwahi hata kuyaota, Nimshukuru M/mungu kwa kunipa Nafasi hii ya kukumbuka Ndugu zangu ambao nimewaacha katika
Eneo hili na kupata nafasi ya kuzungumza nao mawili ,matatu
Ya kuwapa Moyo…!! faraja…!!!!! Mungu anawaona na Maombi yangu yapo kwenu…!!! 🙏 sitochoka
Kuwa nanyi siku zote…!!! Na kidogo
Au kingi changu kiwafikie kama fadhila ambazo ni ngumu
Kuwafikia watu wote..!!! Ila nyie
Mliobahatika kwa leo mkawe wawakilishi wa wengine M/mungu awabariki sana…!!! Ndugu zangu Changamoto, pandashuka, majaribu, zifanye kuwa motisha wa kukufanya uongeze juhudi…!! #MunguHajakuumbaUjeteseka..!! Ipo siku….!!! 🙏🙏