Basata Yamchanganya JDee Juu ya Kibali cha Kusafiria Nje ya Nchi

Malkia wa Bongo Fleva, Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady Jaydee ameonekana kushindwa kuwaelewa Baraza la sanaa nchini (BASATA) kuhusu masuala ya vibali.

Jaydee kupitia mtandao wa Twitter, ameandika swali lake kwa baraza hilo linalodai kuwa kama anahitaji kulipa na kuwa na kibali chochote endapo atataka kusafiri kwenda nje ya nchi kwa shughuli zake binafsi nje ya kazi zake za sanaa.

“Kwahiyo hata kama nasafiri kwenda vacation natakiwa nichukue kibali na nilipe 50k au inakuwaje ? @BasataTanzania au ni wanaoenda ku perform tu . Maana Safari zangu binafsi naenda kama Judith 🤷🏽‍♀️ Je! Pia siruhusiwi kujiamulia kusafiri kama raia wengine?,” ameandika Jide.

Hit maker huyo wa ‘Anaweza’ ameuliza swali hilo kutokana na utekelezaji wa sheria ya msanii kuhitajika kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Baraza hilo endapo atakuwa na safari ya kufanya show) nje ya nchi.

Wiki hii BASATA wametoa tozo mpya ya bei ya vibali kwa wasanii ambao wataenda kufanya show nje ya nchi watatakiwa kulipia kiasi cha shilingi milioni tano.