Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abubakar Chande maarufu kama ‘Dogo Janja’ ambaye pia ni mume wa msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka na kudai sababu kubwa iliyomfanya kushindwa kuzaa nje ya ndoa ni kutokana na wosia aliyoachiwa na baba yake.

Dogo Janja amebainisha hayo baada ya kuulizwa swali na miongoni mwa mashabiki zake waliokuwa wanafuatilia kipindi hicho kuwa ana watoto wangapi hadi hivi sasa.

“Sijawahi kusingizwa mtoto na mwanamke yoyote yule kwasababu mimi napenda sana kutumia kinga, halafu marehemu baba yangu aliwahi kuniambia nisiwe na mtoto nje ya ndoa”, amesema Dogo Janja

Pamoja na hayo, Dogo Janja ameendelea kwa kusema “kwa sasa nimeoa siwezi kuendelea kutumia tena kinga na panapo uzima nitapata mtoto”.

Mbali na hilo, Dogo Janja amesema kupitia ndoa yake imemfanya kukua kiakili katika kufikiria na kutofanya maamuzi mbalimbali na wala hajutii kumuoa mwanamke ambaye amemzidi umri mrefu zaidi yake.