Nina wivu kwa mume wangu akitoka bila mimi lakini…- Mke wa Babu Tale

Wiki weekend iliyopita kwa mara ya kwanza meneja wa Diamond Babu Tale alitoka na mama watoto wake na kwenda kwenye arobaini ya mtoto wa Zamaradi iliyofanyika huko Bunju B.
Bongo5 ilifanya mahojiano na mke wa Babu Tale na kumuuliza anajisikiaje pale anapomuona mume wake akipiga picha na warembo mbalimbali wakati akiwa kwenye shughuli zake za kikazi.
“Wivu upo lakini unategemea upo kwa kiwango gani na wivu ukiuendekeza mtakwama,” alisema mama watoto huyo wa Tale.
Kwa upande wa Babu Tale alidai kwa kuwa yupo kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu amejifunza hawezi tembea na mke wake kila sehemu.
“Leo sijaja kazini nimekuja kwenye shughuli ndio maana unaona niko na mke wangu,” alisema Babu Tale.