Kajala Apigwa Stop Kujirusha Kwenye Kumbi za Starehe

STAA mkali wa filamu Bongo, Kajala Masanja ameifungukia sababu ya kutojirusha kwenye kumbi za starehe hivi karibuni na kudai kuwa kwa sasa yupo kwenye himaya ya mtu ambaye hapendi kabisa mambo ya kutoka usiku.
Kajala alisema watu wengi wamekuwa wakimuuliza kwa nini haonekani kwenye kumbi mbalimbali za starehe lakini kikubwa ni kwamba anamheshimu sana mtu aliyenaye kwenye uhusiano kwa sasa na ndiyo maana ameamua kujituliza.
“Unajua kuna kipindi mambo yanabadilika kabisa na unafanya vitu vingi kulingana na wakati uliokuwepo, mimi sasa hivi nipo na mtu ambaye hapendi kabisa vitu hivyo vya kutokatoka usiku lakini pia hata mimi mwenyewe nimebadilisha maisha yangu siyo yale tena,” alisema Kajala huku akiahidi kumwanika mwandani wake siku zijazo.