Linah Atoboa Siri ya Walipokutana kwa Mara ya Kwanza na Mpenzi Wake

MPENZI msomaji tunazidi kuinjoi simulizi za watu mbalimbali juu ya namna walivyokutana na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi.  Wiki iliyopita tuliwaona mastaa wawili; Aunt Ezekiel na mpenzi wake Moses Iyobo ambaye ni dansa wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Leo tunaye mwanamuziki anayefahamika kwa jina la Esterlina Sanga ‘Linah’ akisimulia namna alivyokutana na mpenzi wake anayefahamika zaidi kwa jina la Shabani au Director Gost. Huyu hapa songa naye; “Nilikutana na mpenzi wangu miaka mitatu iliyopita, nakumbuka siku ya kwanza kabisa tulikutana benki tukiwa kwenye mstari, tulikuwa tunalalamika kuhusu foleni kwa pamoja.

“Wakati huo sikumzingatia mpaka baadaye tulipokuja kufahamiana ndipo aliniambia kuhusu suala hili. Sasa siku hiyo ilipita, siku moja niliposti kwenye Mtandao wa Snap Chart kwamba ninakwenda muvi, kumbe na yeye akaniunganishia ili tu kuja kuonana na mimi.
Tokeo la picha la lina sanga
“Baada ya muvi alinifuata na kuniomba namba ya simu, nilimpa lakini sikumtilia maanani kwa sababu sikuwa hata ninakumbuka kwamba ndio yule tuliyekutana benki, nilifahamu tu ni kati ya mashabiki zangu wengi ambao hunishobokea wakiniona. “Sasa siku zilisonga mbele huku akinicheki mara kwa mara kwenye simu, lakini nilikuwa ninamjibu kwa mkato maana nilimuona ni mtu msumbufu fulani hivi,” anasimulia Linah.

Linah anaendelea kwa kusema, Shaban hakuchoka kumtafuta. Baada ya kuona kila akimpigia simu Linah anajibu kwa mkato hata alipomuomba waonane alimpotezea aliamua kumfungukia kwenye simu kwamba anampenda.

“Kiukweli siku ya kwanza aliponiambia ananipenda nilimpuuzia. Lakini baadaye niligundua ni mtu ambaye alikuwa anamaanisha kile alichokuwa anakisema kwa sababu alikuwa hakati tamaa. “Baada ya kuona hakati tamaa niliamua kumkubalia na kuwa naye, hapo ndipo safari yetu ya mapenzi ilipoanzia.
Picha inayohusiana
“Nilipokuwa naye ndipo nilipogundua mambo mengi. Kumbe jamaa ni mtu ambaye alikuwa ananifuatilia muda mrefu sana. Sikuweza kuamini aliponionyesha posti yake aliyoposti kwenye Mtandao wa Facebook mwaka 2013, kwamba anavutiwa na uzuri wangu na ananipenda sana.

“Pia aliandika kwamba atahakikisha anafanya kazi kwa bidii kuhakikisha anapata pesa na kunipata mimi na hatimaye Mungu ameweza kumsaidia na ameninasa na kunipa mtoto mzuri aitwaye Tracy, ha! ha! haa!,” Linah anafunguka na kucheka. Mrembo huyo anamalizia kwa kusema kwamba anampenda mpenzi wake huyo na wana malengo makubwa kwenye uhusiano.