Nedy Music Aamua Kujibadirisha Macho Aweka Lenz Machoni

Inaweza kuwa ni jambo jepesi kwao pale wanapotaka kujaribu mambo lakini inakuwa inawaweka mashabiki wao katika wakati mgumu sana hasa wanapofanya vitu vyenye utofauti uliopitiliza.

Msanii wa muziki anaofanya vizuri sasa katika muziki Nedy muziki nae amewaacha hoi mashabiki wake baada ya kupiga picha ikimuonyesha akiwa ameweka lenzi ya macho huku swala hilo likizoeleka kuwa ni la wanawake.

Hivi karibuni kumekuwa na tabia ya wasanii wa kiume kufanya vitu ambavyo vinakuwa kinyume na maadili ya jamii lakini pia vinapingana na jinsia zao, hapo karibuni kuli-trend swala la diamond platinimz kuonekana akiwa amevaa kikuku mguuni, leo hii ni Nedy music nae aliamua kuweka lenz .

Ingawa pia sio nedy pekee aliyemua kuja na style hii, pia Country boy katika wimbo wake mpya wa  wanaona haya ameonekana akiwa amefnya hivyo, mambo haya yanawafanya mashabiki kuwatukana, kuwadharau na hata kuwapoteza pia.