Mwanamama asiyeishiwa matukio katika mitandao ya kijamii, Faidha Omary maarufu kama Sister Fey amefunguka na kudai hakumbuki idadi kamili ya wanaume ambao ameshatembea na kwenye mapenzi hadi sasa kwa haraka.

Sister Fey amebainisha hayo baada ya watu wengi kumshambulia kwa maneno kwenye mitandao ya kijamii kuwa anawaibisha wanawake kwa kile anachokifanya kuhusiana na mahusiano yake.

“Kiukweli sikumbuki idadi kamili wanaume ambao nimeshakuwa nao  kwenye mahusiano yangu tangu nilipoanza kujitambua hadi kufika hapa nilipo kwa sasa, ila kwa uchache ninaweza nikasema wanane. Maana wengine siwakumbuki”, amesema Sister Fey.

Mbali na hilo, Sister Fey hakusita kumsifia ‘kibenten’ chake, Elias Njau ‘Holystar’ kuwa ni mwanaume wa pekee duniani kwa madai ameweza kumfanya ajione mwanamke aliyekamilika kwa kupata raha na amani ndani ya penzi hilo.

“Kiukweli tokea nilipojitambua na kuanza kuingia kwenye mahusiano sikuwahi kufurahi tendo la ndoa hata mara moja, wanaume wote ambao niliwahi kuwa nao hawakuwahi kunifanyia hivyo. Holystar ni mtu ‘special’ sana kwangu….

Mara ya kwanza kunitokea hali hiyo nilishindwa kujifahamu kiukweli maana ilinitia uwoga nikajihisi pengine nimepatwa na ugonjwa, lakini nilipoenda hospitalini Daktari aliniambia sina tatizo lolote bali ni jambo la kawaida kutokea wakati wa tendo la ndoa”, amesisitiza Sister Fey.

Pamoja na hayo, Sister Fey ameendelea kwa kusema “Holystar ni mwanaume wa kwanza kwangu kunihudumia yaani kuniachia pesa ya matumizi nyumbani wakati yeye akitoka kwenda kuhangaika. Nilipotoka kote mimi ndio nilikuwa napambana kwa hali na mali ili nimlishe mwanaume niliyekuwa naye pamoja na kumvalisha”.

Kwa upande mwingine, Sister Fey amesema lengo la yeye kuweka mahusiano yake hadharani ni kutaka kuwathibitishia familia ya mpenzi wake huyo, kuwa anampenda kijana wao na wala hana mwanaume mwingine yoyote ili waweze kukubali ombi suala la ndoa yao.