Raisi wa TCCIA bwana Octavian Mshiu akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari. Kulia ni bwana Gotfrid Muganda, kaimu Mkurugenzi WA TCCIA

Chama cha wafanyabiashara,viwanda na kilimo Tanzania ( TCCIA ) leo kimefanya mkutano na wanahabari katika ofisi zake jijini Dar es salaam na kutoa taarifa na muelekeo wake hususan kwa kipindi hiki kinapoelekea kutimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini hapo, Kaimu Rais, Ndugu Octavian mshiu, aliyeteuliwa kukiongoza chama hicho baada ya Rais wake, Ndugu John Ndibalema Mayanja kufariki wiki kadhaa zilizopita, amesema kuwa, TCCIA imefanikiwa kufungua tawi lake la kwanza nje ya nchi, nchini Uturuki na jitihada bado zinafanyika ili kufungua matawi mengi zaidi katika nchi nyingine huku akitoa wito kwa watanzania kujiunga na kufungua matawi ya Chama hicho Ughaibuni.

Kwa sasa TCCIA inatarajia kuunganisha mashirika binafsi na kufanya kazi kwa ushirikiano na vyama vingine vya kibiashara ili kunyanyua uchumi wa nchi na kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika sera ya Tanzania ya viwanda.Raisi wa TCCIA bwana Octavian Mshiu akizungumza na waandishi wa habari

Kuelekea miaka 30 ya Chama hicho, TCCIA imejipanga kushirikiana na vijana kwa kuwekeza nguvu nyingi ndani ya tawi lake la Chama cha vijana ( TYM ) na kuboresha mawasiliano kati ya Makao makuu ya chama na ofisi zake zilizopo mikoani na wilayani. Ili kuboresha huduma hizo, TCCIA inafanya kazi kwa kushirikiana na vyuo vikuu hapa nchini na sasa wameanza na chuo Kikuu cha Dar es salaam-UDSM na Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine-SUA.

Mshiu, anakaimu nafasi hiyo ya Uras ndani ya TCCIA hadi mwezi Novemba utakapoitishwa mkutano mkuu wa Chama cha wafanyabiashara,viwanda na kilimo Tanzania.

SHARE
Previous article
Next articleROSTAM KUONDOKA YANGA