Johari na Ray Mambo si Shwari Kisa Hiki Hapa

Mastaa wahenga Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ wamefika pabaya baada ya kudaiwa kuwa hawana mahusiano mazuri na kila mmoja anafanya kazi kivyake huku Johari akionekana mkoani Mwanza na bwana mpya.

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na mastaa hao, kwa sasa Johari na Ray hawapikiki kwani hata juzikati Johari aliposherehekea siku yake ya kuzaliwa, Ray hakumposti kama ilivyokuwa zamani. “Hivi mnajua kuwa Johari na Ray hawana mahusiano mazuri unaambiwa hata kampuni imesambaratika kila mtu anafanya filamu zake lakini Johari muda mwingi yupo mkoani kwa bwana.

“Sababu kubwa ya kugombana kwao inadaiwa kuwa Ray amemkasirikia Johari kuwa na bwana mwingine licha ya kuwa yeye ana mzazi mwenzake (Chuchu Hans) lakini bado anamuonea wivu Johari,” kilisema chanzo.

Baada ya habari hizo kutua kwenye gazeti hili, mwandishi wetu alimvutia ‘waya’ Ray na kumhoji sababu ya yeye kutomposti Johari na kumueleza madai yote kuhusiana na kutengana kwao, kikazi na kutoelewana ambapo alianza kwa kusema yeye si muumini wa mambo ya Kizungu na wala hana tatizo na Johari.

Ray alidai yeye huwa hasherehekei bethidei yoyote kwa sababu anaamini siku aliyozaliwa alikuwa analia kwa hiyo hawezi kufurahia siku hiyo. “Si unajua siku ya kuzaliwa mtu huwa analia bwana, sasa hivi mimi ni baba naelewa kila kitu siku hiyo nilikuwa nalia siwezi kufurahia kwa namna yoyote ile, ila kwa sababu siku bado zipo basi nitamposti,” alisema Ray.
Tokeo la picha la ray kigosi
Aidha, Ray aliongeza kuwa yeye na Johari hawana ugomvi wowote ule na haelewi ni kwa nini anaulizwa Johari wakati hata watu wengine huwa hawaposti. “Kuhusiana na kazi mimi najua tunafanya kazi kama kawaida hayo mengine siyajui,” alisema Ray.

Baada ya kuzungumza na Ray, Risasi Jumamosi lilimsaka Johari ambaye alisema kwa upande wake ana mambo yake na Ray naye anafanya yake hivyo hapendi sana kuongelea mambo ya watu. “Kama mimi nina bwana huko Mwanza hata yeye ana mpenzi wake hapa Dar mimi naona hayo mambo si vema kuyaongelea,” alisema Johari.

Johari na Ray waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi lakini pia wamekuwa wakifanya kazi kwa pamoja chini ya Kampuni ya RJ ambayo wanashea pamoja lakini kwa sasa inaelezwa kuwa, kila mtu anafanya ishu zake na hakuna tena uhusiano wa kimapenzi wala kufanya kazi pamoja.