Kocha wa Coastal Union ya Tanga amefunguka kwa mara ya kwanza kueleza kwanini aliamua kumsajili Alikiba ambaye ni muimbaji mahiri ya muziki nchini Tanzania.

Akiongea mapema jana baada ya mazoezi, Kocha Juma Mgunda wamedai haikuwa kazi rahisi kupata saini ya mchezaji huyo.

“Tume msajili Ali Kiba kwakuwa anajua kucheza mpira na sio kwasababu anajua msanii mzuri anajua kuimba” Juma Mgunda alisema hayo mara baada ya mazoezi ya jana jioni.

Aliongeza, “Ali ni mchezaji mzuri sana, anajua mpira kama mlivyomuona leo kwenye mazoezi ni mchezaji ambaye ana haki na uwezo wa kuichezea Coastal Union na akaisadia timu”