Victoria kimani Athibitisha Hana Bifu na Wolper
Msanii mkubwa kutoka kenya Victoria kimani aliwahi kunukuliwa hivi karibuni huku akisema kuwa hamfahamu kabisa jackiline wolper na hajawahi kumsikia  kokote.Hali iliyoleta tafran na mashabiki wakaanza kuhojiinawezekana wawili hao wanaweza kuwa na bifu.
Akioneshwa katika kipindi cha break cha Clouds tv moja kwa moja kutoka afrika ya kusini na Kontinyo, kimani alisema kuwa  hamjui kabisa wolper labda apitie google na kumsearch ili aweze kumjua .
baada ya hapo mwanadada huyo alijirudi na kuonyesha kumjua Wolper na kusema anamjua na ni msichana mrembo sana, maneno hayo ya Victoria kimani yalikuja tena kuonekana katika moja ya comment zake katika page ya clouds media.
Mwanadada Jackiline Wolper kwa sasa yuko nchini knya ambapo anataka kufanya jitihada kubwa za kufungua biashara zake za nguo na ujasiriamali wake mwingine nchini humo.