MC Pilipili Amuanika Mpenzi Wake Atakayefunga Naye Ndoa

Mchekeshaji Emmanuel Mathias aka MC Pilipili ametangaza tayari amempata mwenza wake katika mahusiano na hivi karibuni wataingia kwenye maisha ya ndoa.

MC Pilipili akiwa na mpenzi wake.

MC huyo maarufu kwa sasa siku ya jana alikutana na baadhi ya wadau wake kwaajili ya maandalizi ya shughuli hiyo.

Muda mchache baada ya kumalizika, MC huyo alimpost mchumba wake huyo na kuweka kopa ikimaanisha mapenzi.

Pia MC huyo alipost video ambayo ilikuwa inawaonyesha wadau mbalimbali wakijadiliana kuhusu ndoa hiyo.