‘BABA‘ mzazi katika filamu ya ‘Chumu’ aitwaye, Jafari Dionizi amemzungumzia mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ambaye ameapishwa jana ya kwamba nyota yake ya kuwa kiongozi ilianzia katika filamu.

Akipia stori na mwandishi wetu, baba huyo ameeleza kuwa karama ya kuwa kiongozi ilionekana kabla hajaingia katika siasa kwani nyota hiyo ilionekana pale alipokuwa akiongoza mambo mbalimbali mazuri ya filamu na watu kumuelewa.

“Kipaji cha Jokate kuwa kiongozi hakijaanzia ukubwani bali kilianzia wakati akicheza filamu ya ‘Chumu’. Mimi kama baba yake kwenye filamu hiyo sijawahi kugombana naye na hata nikikutana naye akiwa na marafiki zake hunitambulisha kwao mimi kama baba yake, Mungu aendelee kumpa uwezo zaidi wa kushika nyadhifa mbalimbali katika nchi hii,” alisema Jafari.