Kajala Awatolea Uvivu Wanaomjadiri Maisha Yake na Safai Zake za Nje

Msanii wa filamu za Kibongo nchini Kajala Masanja amewatolea povu watu wanaofatilia maisha yake baada ya kuhojiwa juu ya Safari zake za nje ya nchi za mara kwa mara.

Global Publishers wanaripoti kuwa marafiki wa Kajala wamekuwa wakihoji ni wapi Msanii huyo anapata pesa za kusafiri mara kwa mara kwenda Dubai ili hali uwezo wake wanaujua.

Kwa kweli tunashindwa kumuelewa mwenzetu hizi safari zake za kila mara Dubai, anapata wapi hii hela maana kama ni kazi za filamu tunajua sasa hivi soko lilivyo gumu. Kwa kweli mwenzetu sijui ni bwana mpya, sijui ana biashara gani inayomuingizia kipato”.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, alipohojiwa kuhusu tuhuma hizo Kajala aliweka wazi kuwa kinachompa jeuri ni ubalozi pamoja na kazi yake ya sanaa.

Wewe unajua mimi ni balozi, pia filamu sijaacha kuigiza iwe ni za watu au za kwangu, mtu anaanzaje kuhoji safari zangu za nje ya nchi?

Niwashauri wanaoibua hayo maswali kwangu wachape kazi, waache majungu“.