Klabu ya Simba Yatambulisha Jezi Zao Mpya

Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC wametambulisha jezi zao mpya zitakazotumia msimu wa 2018/19.

Kwamujibu wa Mkuu wa habari na mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema kuwa jezi hizo zitaanza kuuzwa rasmi hapo kesho kuanzia majira ya saa 10: 00 alasiri.

Simba wamezitanga jezi hizo ambazo zitatumika kwenye michezo mbalimballi.

Wakati jezi zao nyeupe zitakuwa kwaajili ya mechi za ugenini huku nyekundu zikitumika kwa mechi za ugenini.

Simba imetambulisha jezi hizo zenye nembo ya mdhamini mkuu SportPesa na Mo Energy Drink ambao ni wadhamini wapya waliotangazwa leo kwa kuingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya shilingi milioni 250.