Shirikisho la soka Tanzania TFF leo kupitia kwa Rais wa Shirikisho hilo Wallace Karia limemtangaza kocha Emmanuel Amunike raia wa Nigeria kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.

TFF imetangaza kuingia mkataba wa miaka miwili na kocha Emmanuel Amunike ambaye kabla ya kusaini mkataba kama kocha mpya wa Taifa Stars alikuwa akiifundisha club ya Al Khartoum SC kwa msimu mmoja.

Kama humfahamu kocha Emmanuel Amunike ni kuwa aliwahi kuzichezea timu mbalimbali miaka ya 1990 zikiwemo club za Zamalek ya Misri, Sporting CP ya Ureno na FC Barcelona ya Hispania.