Wasiojulikana Waiba (Wamehaki) Akaunti ya Zari

MJASIRIAMALI na mzazi mwenzake na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’,  yamemkuta mazito baada ya kuibiwa akaunti yake ya Instagram (kuhakiwa )na wezi wa mtandao mapema leo Agosti 6, 2018.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni dakika chache baada ya ku-post picha akimtakia mwanaye Tiffah heri ya siku ya kuzaliwa. Aidha, bado haijajulikana ni hackers wapi wameingilia mtandao huo wa Zari ambao alikuwa na followers zaidi ya milioni 4.2 na kuudukua kisha kufuta kila kitu huku mwenyewe akiwa hajatoa tamko lolote mpaka sasa.
Mastaa kibao wamekuwa wakikumbwa na janga hilo la kuibiwa akaunti zao wakiwemo Shilole, Aunt Ezekiel, Chege, Wema Sepetu, Wolper na wengine kibao.