Mwanadada amanesemekana katika mitandao ya kijamii kuwa kwa sasa amemuweka ndani harmorapa na kumsaidia kwa kila kitu mpka afamilia  yake anajulikana kama khadija ziota kutoka mwanza amefunguka mambo makubwa na mazito kuhusu msanii anaefanya vizuri sana katika tasnia aslay.

Mwanadada huyo anaekiri kuwa aliwahikuwa na mahusiano na wasanii wengi sana na kuwa anawasaidia lakini baadae wanakuja kuachana nae , anasema kuwa aliwahi kuwa na mahusiano na aslay na kumsaidia sana lakini alikuja kumuacaha kwa sababu ya kuchoka kuwa anaombwa pesa kila siku.

Mimi na aslay tulishwahi kutembea, tulishakuwaga wapenzi,tulishafanya vitu vingi tu mbalimbali hata ile nyumba yake ghorofa mimi ndio niliemalizia ile nyumba.tulikuwa tunakutana sana Isamilo lodge na Gold crest, tumelala sana pale.

Alipoulizwa sababu ya kwanini aliachana na Aslay ,mwanadada huyo kwa dharau kabisa alisema kuwa alichoka kuombwa ela na aslay na ndipo alipomuakumuacha.

Tuliachana kwa sababu mapenzi yana mwanzo na mwisho,yaani sikumbuki lini ila anaomba sana ela, unajua mtu ukiombwa saa ela unachoka nikamwamcha.