Msanii wa mziki wa kizazi kipya na mkali wa R&B Tanzania Ben Pol amefunguka mwanzo mwisho kuhusiana na zile tetesi kuwa yeye ana mahusiano na msanii mchekeshaji Ebitoke.

Ben Pol ameongea hayo katika mahojiano aliyoyafanya na Bongo5 siku ya Tamasha la In Love & Money ambalo limeandaliwa na wasanii wawili Jux pamoja na Vanessa Mdee.

Alisema:- “Kuhusiana na mahusiano hayo its Complicated ingawa kila kitu nilishaongea ila kila kitu kilichoonekana kwenye vyombo vya habari ni sehemu ya maisha yangu” na kama yuko na mahusiano na Ebitoke hawezi kuzungumza chochote.

Tetesi za msanii huyu kuwa na mahusiano na Ebitoke zilianza pale mwanadada huyu alipotangaza kupitia vyombo vya habari kuwa anampenda sana Msanii huyo.

huku akimaliza kuwa “vyovyote mtu atakavyohisi aendelee kuhisi ila mimi siwezi kutamka chochote ila muda ukifika kama kweli niko kwenye mahusiano ntaweka wazi na kama siko nae pia itafahamika”