Licha ya Kuwa Mkuu wa Wilaya Jokate Adai Kuwa Atoacha Kuwa Mwanamitindo

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ambaye pia ni mwanamitindo na mjasiriamali amesema hataacha kuwa mwanamitindo kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Jokate amesema baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali juu ya hatima yake ya uanamitindo na hivyo amewatoa wasiwasi kuwa hawezi kuacha.

Amesema ataendelea kuvaa nguo za wabunifu mbalimbali. “Jamani mimi bado mrembo hivyo sitaacha kuwa mwanamitindo sababu ya kuwa mkuu wa wilaya,kwani bado navaa nitaendelea nayo, nitavaa vitenge, nguo mbalimbali ambazo zinaweza kubuniwa, ila kwa sasa lazima kuwe na utaratibu wa mavazi lazima nibadilike kidogo, nivai kama mtumishi wa umma.

“Lakini pia ikumbukwe kuna mitindo mbalimbali mafuta, wanja ni urembo lazima tuendelee nao sababu ni maisha ya kila siku, sio kama nitashiriki sana ila nitashiriki kama uwezo nitakuwa nao kuvaa mitindo inayobuniwa na wanamitindo mfano kama hii nguo niliyovaa imebuniwa na mwanamitindo wa kitanzania nitaachaje urembo bwana, nitaendelea kusapoti mitindo na huu huu ukuu wa wilaya wangu,” alisema Jokate.

Jokate pia alisema kuwa,hakuwahi kufikiria kama atakuwa mkuu wa wilaya japo alikuwa na ndoto ya kuwa kiongozi na kwa upande wa siasa alikuwa anatamani kugombea nafasi ya ubunge.