Msanii wa muziki Bongo, Nandy ameshinda tuzo kutoka Maranatha Awards. Hizi ni tuzo maalumu kwa ajili ya muziki wa Injili ambazo hutolewa nchini Kenya.

Sasa Nandy ameshinda katika kipengele cha Best Worship Song Cover, kupitia wimbo wa Angel Benard unaokwenda kwa jina la Nikumbushe Wema Wako.

Hii ni tuzo ya pili kwa Nandy mara baada ya usiku wa November 12, 2017 kuibuka mshindi kupitia All Africa Music Awards 2017 (AFRIMA) zilizotolewa nchini Nigeria katika kipengele cha cha Best Female Artist In Eastern Africa Award.