Ndoa Ya Abdu Kiba Yadaiwa Kupumulia Mashine

Ndoa ya staa wa Bongo fleva Abdu Kiba ambaye ni Kaka wa Ali Kiba imedaiwa kuwa katika hali mbaya na kuwa mbioni kuvunjika.

Ndoa hiyo na Abdu Kiba na mkewe Rwahida imeendelea kuwa matatani ambapo imesemwa kuwa Abdul Kiba mara nyingi amekuwa ni mtu wa kurudi nyumbani usiku na mara nyingi anashinda maskani maeneo ya Ilala Mtaa wa Arusha, kitu ambacho mkewe huyo amekiona kama sio sawa na pamoja na hayo bado anaona hakuna upendo ndani.

Baada ya Tetesi hizo gazeti hilo lilimsaka Abdu Kiba ili kupata ukweli wake lakini mara moja aliwataka wazungumze na Meneja wake ambaye mara moja alifunguka:

Hizo habari hata sisi tumezisikia kwamba watu wanasema hivyo lakini naomba kukuhakikishia hakuna ukweli wowote.

Unajua Abdul ni tofauti sana na Ally, yeye mara nyingi anapenda sana kuwa huru sana hivyo watu wakimuona pekee yake wanafikiria hivyo lakini sivyo au wengine wanasema kwa nini hamposti mkewe…”.

Lakini pia na mke wa Abdu Kiba, Rwahida amefunguka na kusema:

Hakuna ukweli wowote mimi na mume wangu tupo vizuri tu kama kawaida hakuna kitu kama hicho“.