Baada ya Kundi la Muziki la Hip Hop @romastamina linaloundwa na Rapa @roma_zimbabwe Pamoja na @staminashorwebwenzi kufika Baraza la Sanaa Leo, Msanii Roma ameamua kutoa ujumbe ambao amewaandikia BASATA Kutokana na Wimbo wao Mpya Unaoitwa #PARAPANDA

Kupitia Page ya Roma ya Twitter ameandika Kuhuzunishwa na Mwenendo wa Baraza la Sanaa na Kuonesha Kuchukizwa na Maamuzi ambayo yamekuwa yakifanywa na BASATA.

Katika Tweet hiyo Roma ameandika kuwa Baraza hilo linaua Sanaa, Ubunifu na Kipaji na kumalizia kuwa yeye hachukizwi na Sanaa ila anachukizwa na Utendaji Kazi kisha akawauliza pia Mashabiki zake kutoa Maoni juu ya wimbo huo kama una matatizo yoyote.