Shamsa Ford Atoboa Siri ya Safari ya Sauz kwa Wanakamati Walioalikwa Kwenye Birthday ya Tiffa ' Hakuna Safari Kiki Tu na Hata Ingekuwe Nisingeenda"

Shamsa Ford Atoboa SIRI ya Safari ya SAUZI ya Wanakamati  ambayo wameshughulikia maandalizi ya King Salah 40 ambaye ni mtoto wa Zamaradi kwenda Afrika Kusini kwaajili ya kuhudhiria Birthday Party ya Tiffah.

Shamsa ford amesema kuwa hadi leo augost 6 ambayo ndo siku ya birthday ya mtoto huyo akuna taratibu zozote za safari zilizoanza kufatiliwa kama passport kwaajili ya kufika huko south kwenye part hiyo na hadi sasa ajui lolote kama hiyo safari ipo kweli.

“Yani hadi leo sijui lolote mi ninavyoona ilikua ni Kiki tu si unajua tena wasanii na ingekuwa ni kweli ungeona hata baadhi ya wanakamati wakipost kuhusu safari ila adi sasa hakuna mwanakamati hata mmoja aliyepata hata tiketi lakini hata ingekuwa kweli nisingeenda kwasababu sina urafiki nao nikienda kule nitaongea nae nini” Shamsa Ford