Uchebe Awapiga Mkwara Wanaomnyemelea Shilole " Ole Wake Nimkute Mtu Anamnyemelea Shilole"

CHIMBA mkwara! Mume wa mwanamuziki wa miondoko ya mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Ashrafu Uchebe ametangaza vita kwa mwanaume yeyote ambaye atamkuta na mkewe kimapenzi kwani yuko tayari kwenda jela endapo atamkuta mkewe na mwanaume mwingine au kumfumania.

Uchebe alisema kuwa anajua anapata tabu gani kuhakikisha anailinda ndoa yake hivyo ataumia sana atakapomkuta mwanaume mwingine anamrubuni mkewe na anaweza kufanya kitu ambacho hakikutarajiwa na watu wengi.

“Mimi nampenda sana mke wangu najua wazi ni kiasi gani naumia kuilinda ndoa yangu isiingiliwe na kidudu mtu ila watu hawezi kuelewa hata kidogo hivyo kama nitamkuta mwanaume yeyote au nikimfumania mke wangu huyo mwanaume ama zake ama zangu,” alisema Uchebe.