Ni Siku moja tu imepita Msanii na Video Vixen Maarufu kwenye Game ya Bongo Fleva @amber___lulu kuweka Picha ya PakaRapper @youngdaresalama Kwenye Page yake ya Instagram na kuporomosha ujumbe wa kimafumbo ndani yake ikiwa kama sehemu ya kupromote kazi yake mpya aliyoitoa hivi karibuni iitwayo #MACHOZI

Leo Rapa Young D nae ameamua kuandika ujumbe mzito kwa Mrembo huyo na kuwaonya kina dada wengine wanaofanya kazi ya sanaa kutafuta kiki ili kuzisogeza zaidi kazi zao kwa mashabiki ambao wanawafuatilia.

Kupitia Page ya Instagram ya Rapa huyo ameandika kuwa ” Kina Dada mnaofanya mziki ningewashauri kutumia mziki wenu zaidi ya hizi kiki za kufosi. Kama wimbo wako unaona haufanyi vizuri rudi tena studio toa mwingine sio kunitumia mimi kwa upumbavu wako. Niko na mpenzi wangu namuheshimu sana huu utoto nilishamalizaga! ”

JE, UNAHISI KUNA KITU GANI KINAENDELEA KWA WAWILI HAWA ? AU NI KIKI PIA YA KUSOGEZA MJINI KAZI HIYO MPYA YA #MACHOZI ?