Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo tarehe 8, Agosti 2018 amemtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo alimjulia hali na kumpa pole kufuatia ajali ya gari aliyoipata Agosti 4,2018 huko Manyara.