Steve Amkataa Mama Kanumba

Msanii wa filamu bongo ambaye pia ni mchekeshaji maarufu Steve Nyerere, amedai hawezi kuendelea kubishana na Mama Kanumba kwenye vyombo vya habari na mitandaoni kwa kuwa huyo ni mama ambaye anamuheshimu kupita maelezo.

Steve ametoa kauli hiyo leo Agosti 08, 2018 wakati akizungumza na www.eatv.tv baada ya kuenea video mitandaoni ikimuonyesha mama wa Kanumba akitoa kauli zenye utata juu ya Steve Nyerere.

Miongoni mwa kauli hizo za Mama Kanumba ni zilizoweza kuzua gumzo kwenye mitandao ni ‘Steve Nyerere kama angekuwa ananipenda na kunikubali ningeshangaa maana alikuwa hapatani na mwanangu enzi za uhai wake kwa hiyo mimi sioni ajabu kwa yeye kutonikubali

‘Steve ni msaliti sana maana enzi za Kanumba aliwachonganisha na Ray Kigosi hadi wakawa hawapatani. Ray na Kanumba walikuwa wanaishi kama ndugu kabisa vile lakini Steve aliingilia kati. Nakumbuka ilikuwa kipindi cha Kwaresma tulikaa familia zote mbili ili kusudi wapatane lakini Ray kwa kinywa chake mwenyewe alikiri kuwa Steve Nyerere ndio mchonganishi”.

www.eatv.tv ilipomuuliza muhusika ambaye ni Steve Nyerere juu kauli hizo zilizotolewa na Mama Kanumba, amesema hayupo tayari kuzungumza juu ya jambo hilo kutokana na kumuheshimu mama huyo.

“Hayo sitaki kuongelea yule ni mzazi, na mimi nimeshamwambia kuwa yeye ni mama. Mimi siwezi kubishana naye kwenye vyombo vya habari maana mama anahisia zake na vitu vingi kiukweli siwezi kuzungumza mengi juu ya hilo”, amesema Steve.

Hii sio mara ya kwanza kwa Steve Nyerere na Mama Kanumba kuanza kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii na mahojiano mbalimbali katika vituo vya habari, kwani hata kipindi serikali ilipofanya mabadiliko ya adhabu ya kesi ya Lulu.

Mama Kanumba alitoa lawama zake kuwa hakupendezewa na mabadiliko hayo na kusababisha Steve naye kumjibu kwa maneno ambayo sio mazuri hadi kufikia kusema amefuta namba zake za simu