Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana na Ajira), Mh. Anthony P. Mavunde ameeleza kwamba Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kustawi kijamii,kisiasa na kiuchumi.

Mavunde ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuujulisha umma wa watanzania kwamba maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Kimataifa ya Vijana kwa Tanzania yatafanyika mkoani Arusha.

Mh. Mavunde alisema maadhimisho hayo yatafanyika tarehe 12 Agosti, 2018 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘MAZINGIRA SALAMA KWA VIJANA’

“Natoa wito kwa vijana wote nchini, wazazi na wadau wa Vijana washerehekee siku hii muhimu ili kwa pamoja tuonyeshe na kutambua umuhimu wa vijana kama washiriki wa Maendeleo ya nchi yetu, aidha nawaomba Vijana wote Tanzania wajitokeze na kushiriki katika Maadhimisho haya ili kwa pamoja tuweze kushirikiana na kujadiliana njia na mbinu mbalimbali za kupunguza changamoto zinazowakabili Vijana” alisema Mavunde.