Sifikirii Kabisa Kutoa Penzi Langu kwa Mwanaume wa Nje ya Nchi- Wolper

STAA wa filamu ambaye pia ni mbunifu wa mavazi, Jacqueline Wolper, amefunguka kuwa kamwe hawezi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi tena na mwanaume ambaye siyo raia wa Tanzania kwa sababu kuna mengi alijifunza kipindi cha nyuma.

Wolper alisema kama ni kumpata mpenzi ambaye anaamini atamfaa basi lazima atoke ndani ya nchi yake japokuwa kuna watu walianza minong’ono kuwa alipokuwa nchini Kenya hivi karibuni, alikuwa na mpenzi raia wa nchi hiyo.

“Sifikirii kabisa kutoa penzi langu kwa mwanaume ambaye siyo raia wa nchi yangu kwa sasa kwa sababu huko nyuma nilipitia huko lakini sasa sihitaji tena kama nimeamua kupendana na mwanaume basi atakuwa ni wa nchi yangu tu,” alisema Wolper ambaye huko nyuma alishawahi kutoka kimapenzi na raia wa Kongo.