Bonge la Nyau Afunguka Kutoka na Khadija Khopa

MWANAMUZIKI Lameck Philipo ‘Bonge la Nyau’ amefunguka kwamba siri ya yeye kuamua kufanya kazi na mwanamuziki mkongwe wa Taarab, Khadija Kopa ni kuleta ladha tofauti kwenye muziki mbali na vile watu walivyozoea.

Bonge la Nyau alisema kwamba kwa ujio huo ambao siku yoyote kuanzia sasa atauachia atawapa nafasi mashabiki wa muziki wake na wale wa Taarab kufurahia muziki mzuri na kuona namna ‘chemistry’ ya Hip Hop na Taarab inavyoweza kufanya kitu ‘amaizing’.

“Watu wanaweza kufikiri nimefanya Taarab pia kwenye kolabo yangu na Khadija Kopa, lakini si hivyo, tumefanya kitu tofauti na kitaleta matokeo tofauti kwenye gemu ambayo yatawashangaza wengi,” alisema Bonge la Nyau.