Harmonize Alivyofichwa Msikitini Tanga Kuhofia Usalama Wake

Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize aka Konde Boy amelazimika kufichwa ndani ya msikiti wa Chuda kwasababu za kiusalama kufuatia idadi kubwa ya watu kumzonga wakati mwili wa Mzee Majuto ulipokuwa ukiswaliwa.
Harmonize hii leo amefika kwenyemazishi hayo jijini Tanga mara baada ya Diamond kuonekana katika tukio la kuuaga mwili wa Mzee Majuto hapo jana Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa kutoka jijini Tanga zinaeleza kuwa, Harmonize ametolewa kwenye eneo hilo kupitia gari la Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela.