Wakati kikosi cha Simba kikiwa katika maandalizi ya kujiwinda na mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Mtibwa FC, kuna uwezekano mkubwa ikamkosa Nahodha wake, John Bocco.

Simba itashuka dimbani kukipiga na wakata miwa hao wa Morogoro katika mchezo wa Ngao hiyo Agosti 18 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kuelekea mechi hiyo imeelezwa kuwa Bocco hajapewa nafasi kubwa ya kucheza kutokana na kutokuwa fiti kiafya kwa ajili ya kucheza.

Ikumbukwe Bocco aliukosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Asante Kotoko Agosti 8 katika tamasha la Simba Day ambalo lilimalizika kwa sare ya bao 1-1 pamoja na jana dhidi ya Namungo FC huko Ruangwa, Lindi.

Aidha, taarifa za ndani zinasema Bocco anaweza akawakosa pia Tanzania Prisons, mechi ambayo itakuwa ni ya ufunguzi wa pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Agosti 22 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.