From @faizaally_ – Nimefikiria jambo hili kwa muda na nimeona nilazima nijirizishe kwa kusema haya @stevenyerere2 amekua akichekwa na kuzaraulika halafu wasanii wamekaa kimya ni kama vile hawajui umuhimu wa uwepo wake , kiukweli sijaona mwanaume bongo movie mwenye uwezo wa kusimamia chochote kama anavyo simamia Steve pindi linapotokea jambo la wito na si msiba peke yake ! Ni nani anaweza kusimama na si kusimama tu na kutafuta hela na michongo ? Na of course bongo movie ni kitu kikubwa kinahitaji mtu kama Steve ni muhimu na nafasi yake ni kipekee inatakiwa iheshimike na zaidi anahitajika.sasa anapopata kashfa na mkaa kimya zaidi mnamcheka ni sawa hivyo ? Wangapi amewsaidia kupata dili za kampeni ? Wangapi amewaombea michango ya matibabu ? Wangapi amewapa connection za hela ? Misiba mingapi amesimama nani angefanya ? na mpaka sasa anachekwa anatengenezea vikatuni vya dharau wote mko kimya .kwa nini msisimame na kukanusha shutuma anazopata ? Hali yakuwa mnajua wengi wenu maskini na mnamuhitaji ?Ndio atakua bora pale msaada wake unapo hitajika ?