Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Monduli Mjini (pichani kushoto), Isack Joseph amejiuzulu nafasi hiyo, kujivua uanachama na kukihama chama hicho kisha kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Isack na viongozi wengine zaidi ya 31 wa ngazi ya Wilaya na Kata wamejiunga na CCM leo Agosti 11, 2018 ikiwa ni wiki chache baada ya aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Monduli, Kalanga kuhamia CCM. Viongozi hao wamepokelewa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru.

Aidha, wakati wa kuhama, Isack ameehoji yeye ni nani hata asiwe miongoni mwa watu 200,000 wa Monduli wanaomkubali Rais Magufuli