WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amezindua Bonanza kubwa la amani katika uwanja wa mpira wa Sabasaba, mjini Bunda mkoani Mara.

Bonanza hilo ambalo linatarajiwa kufanyika nchini nzima limezinduliwa mjini Bunda na baadae litafanyika nchini nzima likiwa na lengo kuu kutangaza amani nchini.

Akizungumza kabla ya kulizindua Bonanza hilo, Waziri Lugola alisema, michezo inaleta amani michezo inaleta ushirikinao, michezo inaimarisha undugu, michezo inaimarisha ushikamano na michezo uepusha wananchi wasijiingize katika uhalifu, hivyo Wizara yake inatarajia Bonanza hilo litazidi kudumisha amani zaidi.

“Michezo ikiimarishwa tunaimarisha amani, tukishiriki michezo kama hivi wanaokuja kutazama na nyie mnaocheza,  hivyo muda mwingi tunautumia katika kufurahi pamoja na ndio mana vitendo vya uhalifu vitapungua kwasababu watu tunataka tuwe wamoja kupitia michezo,” alisema Lugola.

Waziri Lugola aliongeza kua, Bonanza la kuhubiri amani sio kwamba linafanya wilyani Bunda bali litafnyika nchi nzima likiwa na lengo la kuwaweka watanzania pamoja ili amani nizidi kudumu.

“Hapa tulipo ni uwanja wa CCM na hii ilani ni ya CCM na katika ibara ya 160, 161 na 162 inazungumzia kuimarisha na kudumisha sekta ya michezo, hivyo tupo hapa kutokana na ilani hii ya CCM na lengo kuu ni kudumisha amani,” alisema Lugola.

Waziri Lugola yupo wilayani Bunda mkoani Mara kwa ajili ya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ndany ya jimbo lake la Mwibara wilayani humo.