Msanii wa Bongo Fleva ,Enock Bella amefunguka na kumchana muimbaji mwenzake Beka Flavour kuwa hawezi kumsaidia katika kumuinua kimuziki, kwa madai wote wapo kwenye ‘level’ moja, hivyo sio rahisi kwa yeye kusaidiwa

Enock Bella amebainisha hayo na kusema hajui ni msaada gani ambao Beka Flavour ataweza kumsaidia katika kumtoa kimuziki kama anavyojinadi kwenye ‘interview’, mbalimbali anazokuwa akihojiwa.

“Simshangai Beka kuzungumza hivyo kwasababu na yeye anatafuta ugali. Sidhani kama anaweza akawa na msaada mkubwa wa kunipatia mimi niweze ku-survivor katika muziki wangu kwasababu mimi na yeye tunalingana. Vitu vingine watu wapo kwaajili ya kujitafutia faida kwa kuongea mambo ambayo hayawezekani kufanyika”, amesema Enock.

Pamoja na hayo, Enock ameendelea kwa kusema kuwa “kukaa kimya kwangu haimaanishi nimeushindwa muziki, mimi nina ngoma nyingi ndani zaidi ya albamu, lakini kila jambo lina misingi na sababu zake. Muziki mimi ndio maisha yangu hivyo siwezi kuacha, na hata nikionekana nipo kimya basi watu wajue nina mambo mengine nafanya”.

Kwa upande mwingine, Enock Bella sio rahisi kwa yeye kutoa ngoma kila mara kwasababu kila jambo katika muziki wake huwa analisimamia yeye binafsi, na hakuna wa kumpa ushirikiano kwa jambo lolote lile kama ilivyokuwa kwa wenzake.

Tokea lilipovunjika kundi la Yamoto Band miaka michache iliyopita, ilipelekea kila msanii aliyokuwepo katika kundi hilo, kufanya kazi kama ‘solo artist’, lakini kwa bahati mbaya hawakuweza wote kwa pamoja kupokelewa vizuri katika jamii licha ya awali walipokuwa kama kundi, walipendwa wote.

Enock Bella ni miongoni mwa wasanii waliokuwa wanavutiwa na wengi kipindi hicho, katika kundi la Yamoto Band kutokana na uzuri wa sauti yake ya ‘base’ lakini lilipokuja kuvunjika kundi hilo, ili mchukua muda mrefu hadi alipokuja kutoa kazi yake ya awali lakini hakuweza kupata mapokezi mazuri kwa kile walichokidai wadau wa muziki kuwa anauoga wa kufanya kazi ya pekee yake bila ya kundi kutokana na sauti yake