From @munalove100 – Hii ndo Picha ya Mwisho na Mwanangu, Ila jamani ninapomkumbuka Mtoto wangu Mniache tu napokea matusi kejeli

Yote najua ni Shetani na sina wakumlaumu ila Mungu baba ndo anajua mapito niliopita na mwanangu,njia nilizopita na niliyoyafanya ili mwanangu aishi vizuri na Furaha na nilijitahidi kama Mama kumfanya mwanangu aishi vizuri na kusoma na ata alipoumwa niliteseka na mwanangu kila nilichoambiwa ukifanya hivi atakua sawa nilifanya Lakini badae Mwanangu alipofariki Kila mtu aliongea lake, wakunitukana , wakunikejeli,wakunicheka kua ndo nilichokua naringia kimeshachukuliwa, sijui nilikua napata pesa kupitia uyu mtoto

Mambo Mengi sana niliitwa Malaya na Hata familia yangu iliungana Kuniumiza zaidi na ikiwa maneno yanaendelea kua ntakufa na Lengo lilikua ni Mimi kua nichafuke na kuzalilika na ikiwezekana kufa Nyie mlikua mashuhuda wa kila kitu

Sasa naomba niwape Ushuda na Ukuu wa Mungu pale unapomuacha Yeye afanye kazi na Ukaomba msamaha kwajili ya wale Watu au Adui Anavyokupangia .

Mungu kwanza Alinijaza Roho Mtakatifu nilikua Kila nachoona Mitandaoni siumii wala Sioni ajabu Nilikua nasali Muda Wote na Mungu Alikua anaendelea Kunionyesha Ukuu wake Nakua Yeye Ni Mungu Wa upendo Walitokea watu Kunisaidia Ata sikuwaza Mimi ndo nilichagua Mtoto aje Lini.

Na pia Kila sehemu Kila kitu Kilikua kinapatikana Kwa wakati, wakati kutoa Maiti nchi tofaut na yako kuna milolongo Mingi , ila Mungu alionekana Kwa hilo na nilikua nashangaa nakujiuliza Mungu Kwanini sikukujua mapema .

Nikaona Mungu alikua anasababu maalumu ya kumchukua Mwanangu ili anitengeneze kupitia ilo na Amjui kuna vitu vingine vilibidi vinikute ili nilipe Deni na mimi nilivyo kua Duniani nilitenda wenzangu kwaiyo yaliyonikuta yapo mengine nilikua nalipa Deni ila Mungu si kwamba alikua anipendi .

Na Roho Mtakatifu aliniongoza sawa sawa na Mapenzi yake na Mungu nilizidi kuona Ukuu wake na mpaka leo hii nauona Ukuu wake niwambie tu ndugu zangu Maisha yangu mimi na Mwanangu ya kawe darasa kwenu na Muamini Mungu yupo na anatenda Miujiza mikubwa .Ingawa bado natukanwa sana ,Wanaonichamba wanavyojisikia wanamichamba Mimi sijal kwakua namwamini MUNGU.